Friday 14 June 2013

BAJETI ZA AFRIKA MASHARIKI






 Bajeti za nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zilitangazwa jana zikitoa vipaumbele katika masuala ya usalama, afya, kilimo, elimu, nishati na kuboresha miundombinu.
Bajeti hizo zilizotangazwa na mawaziri wa fedha wa nchi hizo sambamba na ile ya Tanzania, ni za Uganda, Rwanda na Kenya ambayo iliongoza kwa ukubwa wa bajeti.
Bajeti hizo zilitofautiana kwa kiasi kikubwa kutokana na mahitaji na vyanzo vya mapato kwa kila nchi.
Mwelekeo wa bajeti hizo pia umelenga kuongeza mapato kupitia vyanzo vya ndani kwa kuongeza ushuru na kodi kwenye vileo, vyombo vya usafiri na bidhaa za anasa.
Kenya Sh28.5 trilioni
Waziri wa Fedha wa Kenya, Henry Rotich alisema kwamba Bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2013/14 itafikia Sh1.5 trilioni za Kenya (sawa na Sh28.5 trilioni za Tanzania).
Bajeti hiyo ilisomwa jana bungeni jijini Nairobi, ndiyo ya kwanza kwa Rais Uhuru Kenyatta aliyechukua madaraka hivi karibuni.
Moja ya ameneo muhimu yaliyopewa kipaumbele katika bajeti hiyo ni elimu, ambapo Sh17.4 bilioni (Sh330.6 bilioni za Tanzania) zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha mkakati wa Serikali ya Jubilee wa kununua kompyuta ndogo 1,300,000 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi.
Uganda Sh7.2 trilioni
Waziri wa Fedha wa Uganda, Maria Kiwanuka ametangaza Bajeti ya Serikali ya nchi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2013/14 ambapo ambapo Sh 12 trilioni (sawa na Sh7.2 trilioni za Tanzania) zitatumika.
Bajeti hiyo inategemea vyanzo vya ndani vya mapato baada ya misaada ya wafadhili kushuka kwa zaidi ya asilimia 93, kutoka Sh749 bilioni (za Uganda) mwaka 2012/13 hadi Sh50 bilioni za Uganda mwaka 2013/14.
Kiwanuka alisema katika mwaka huu wa fedha, wafadhili wamesaidia asilimia 25 ya bajeti ya nchi hiyo lakini katika mfumo wa mikopo na kufadhili miradi, ambapo matumizi ya Serikali yatafikia Sh8.4 trilioni za Uganda.

SUGU AMPA SHAVU LADY JAYDEE NA ZITTO KABWE KWA MWANA FA





 Ile the Big Square 1, show za magwiji wa muziki Tanzania mwana FA ‘The Finest’ na Lady Jay Dee ‘Miaka 13 ya Lady Jay Dee’ zitapigwa kesho June 14, huku presha ikiwa inaongezeka hasa kwa fans wanaotamani kuhudhuria show walioichagua na kuona ukubwa wa show kama walivyotarajia.


Show hizi kubwa zina nguvu sana kutokana na ukubwa wa majina ya wasanii husika. Kwa mujibu wa lady Jay Dee timu anaconda kesho itaungwa mkono na mheshimiwa Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.

Jide ambae hivi karibuni ameachia wimbo mpya unaopatikana kwenye album yake ‘Nothing but the truth’ inayoitwa Yahaya, amepost kupitia kupitia ukurasa wake wa facebook na pia katika akaunti yake ya Twitter kuonesha list ya wasanii watakaopanda jukwaani, na pia uwepo wa Sugu.

” Miaka 13 ya Lady JayDee, Ijumaa ya kesho shughuli inaanza rasmi saa 3:00 usiku...Ukiskia paaaa ujue show imeisha

1. Prof Jay 2. Juma Nature 3. Grace Matata 4. Hamza Kalala 5. Wakazi na ugeni wa Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a SUGU

Nyimbo zote unazozipenda zitalia tar 14 June, pale Nyumbani Lounge sababu yaaaaa sababu yaaaaaa ?????????”

 Kwa upande wa Mwana FA ambae atapiga show yake na Live band akiwa na kundi kubwa na maarufu kwa upigaji wa Live Band ‘Wananjenje’, yeye amepewa full sapoti na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto kabwe.
Zitto ameweka wazi kupitia akaunti yake ya twitter kuwa anamsapoti sana msanii huyo.

“You have my full support “@MwanaFA”

Thursday 13 June 2013

LANGA AMEFARIKI


Langa Kileo (msanii wa Hip Hop Tanzania, pichani) amefariki dunia leo hii.

Langa alipelekwa hospitali akiwa hajitambui. Anadaiwa kuwa alikumbwa na Malaria kali sana, Hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili jana.

Uchunguzi wa chanzo cha kifo chake bado unaendelea.

Msanii Langa aliwahi kutamba na kikundi cha Wakilisha pamoja na witness na sara ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa bongo flava nchini Tanzania.

Mungu amrehemu.

***************
Post yake kumwaga Ngwea kwenye Facebook ilikuwa hivi:


***************

Na,
===============
Kwa wasiomjua Langa


Je, unamkumbuka Langa Kileo? Bila shaka hili ni jina maarufu, hasa kwa wadau wa masuala ya burudani wa ndani na nje ya nchi.

Huyu ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha.

Mbali ya Langa, wengine ni Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwaijaga `Witness’. Huo ndio uliokuwa mwanzo wa kung’ara kisanii kwa wakali hao, ingawa kwa sasa kundi hilo limesambaratika, kila mmoja akitamba kivyake.

Lakini kwa bahati mbaya, mmoja wao, Langa kwa miaka ya hivi karibuni hakusikika kabisa, jambo lililomlazimu mwandishi wa makala haya kumtafuta sababu za ukimya wake.

Haikuwa kazi rahisi, lakini hatimaye Langa alipatikana na bila kutafuna maneno alisema kwamba, alishindwa kufanya kazi baada ya kuwa `teja’ aliyekubuhu.

Yaani alizama katika matumizi ya dawa za kulevya kiasi cha kupoteza kabisa mwelekeo si wa kisanii pekee, bali hata kimaisha.

“Siyo siri, kilichokuwa kimenifikisha katika hali hiyo ni dawa za kulevya. Kwa miaka mitano nilitumia sana Cocaine, Heroin, bangi na pombe. Namshukuru Mungu sasa nimerejea katika hali yangu…

“Siamini kama nimenusurika kwa sababu madawa yalinitesa, nikafanya mengi ya ajabu yaliyoichukiza familia yangu na marafiki ikiwa pamoja na kuwa mwizi na mkabaji mitaani na nyakati za usiku,” anasema Langa ambaye kundi lao la Wakilisha lilitamba na nyimbo kama `Unaniacha Hoi’ na `Kiswanglish’.

Anaeleza kwamba, kwake hayo ndiyo aliyoyaona maisha yanayomfaa, akidai awali alikuwa amechoshwa kuishi kwa masharti kutoka kwa wazazi wake waliokuwa wanampa mwongozo wa maisha, lakini bila kujua akadhani `anachungwa’.

Kwamba, umaarufu na ngekewa ya kuzishika pesa katika umri mdogo kupitia muziki vilimtia kiburi zaidi, na hivyo kuamua kujitenga kabisa na familia yake iliyomlea kwa mapenzi mazito.

“Niliamini naweza kujitegemea kupitia kazi yangu ya muziki, nikajichanganya mtaani,” anasema kijana huyo aliyetoa kibao chake cha kwanza, Matawi ya Juu mara baada ya kusambaratika kwa kundi la Wakilisha kutokana na kila mmoja kuamua kujitegemea kimuziki. Na kweli, Matawi ya Juu ilidhihirisha kuwa Langa ni moto wa kuotea mbali katika fani. Aliweza kusimama kwa miguu yake na kutikisa.

Mwenyewe anasema: “Jina hilo la Matawi ya Juu lilidhihirisha hivyo pale video ya kibao hicho ilipotajwa kuwania Tuzo za MTV Base kwa upande wa hapa Bongo miaka michache iliyopita, kisha kutwaa Tuzo ya Kisima nchini Kenya. “Moto huo uliwafanya baadhi ya wasanii wakongwe katika gemu ya Bongo Fleva kunitafuta na kunipa majukumu ya kushiriki katika kazi zao, ikiwemo Chagua Moja ya Farid Kubanda `Fid Q’.

“Baada ya kuona wakongwe wamekubali vitu vyangu na kuanza kunishirikisha…nikapata pia safari za nje ya nchi. Huko Nairobi (Kenya) niliweza kufanya kazi na vichwa vikali vinavyounda Kundi la Necessary Noise, Naaziz na Wyre (Kevin Wyre)….”

——————————————————————————–

Anasema mafanikio hayo yalimtuma kufyatua albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la Langa, akiamini itampaisha zaidi kimaisha na kimuziki. Hata hivyo, mambo yalikwenda kinyume. Anasema alipoipeleka sokoni, wauzaji wakubwa waliigomea, hivyo kumpa wakati mgumu wa kuwaza na hatimaye kujikuta akiongeza kasi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Siyo siri, kugoma kwa albamu yangu sokoni kulichangia kasi ya kutumia dawa za kulevya…niliona ni njia pekee ya kuondoa mawazo kwa sababu kazi iligoma, na home (nyumbani) nilishaharibu.

Sikufanya tena kazi kwa umakini na kila kazi niliyoitia haikufanya vizuri….” Anasema kwamba, baada ya mambo kumwendea mrama, ndipo alipoanza kuiba vitu nyumbani kwao kwa lengo la kuviuza na inapotokea amekosa, alidiriki hata kupiga debe katika vituo vya mabasi ili mradi apate fedha za kununua `unga’.

Haikuishia hapo, kwani anasema alijiingiza katika kundi la wahuni waliojihusisha na wizi na ujambazi. “Kwa ujumla nilipoteza mwelekeo. Maisha yangu yakawa ya kutembea na kisu kama kitendea kazi changu katika wizi,” anasema huku akitikisa kichwa kama ishara ya kujutia matendo aliyoyafanya kwa msukumo wa madawa ya kulevya. Anakumbuka akiwa mtumwa wa `unga’, aliingia katika mikasa kadhaa ikiwa pamoja na kupigana na polisi baada ya kunaswa na dawa hizo haramu.

Katika wizi, chochote alichokikuta mbele yake kilikuwa halali. Anasema alikwapua vitu magengeni, madukani na hata magari yaliyoegesha vibaya alinyofoa vioo na mashine zinazosaidia kupandisha na kushusha vioo ndani ya gari.

“Ni matukio ya aibu. Yanasikitisha…,” anasema Langa anayedokeza kwamba, akiwa mtumiaji wa `unga’, alikuwa anakutana na wasanii na watu wengine mashuhuri. Hata hivyo anakataa kuwataja, akidai ni siri yake. `Ufufuo’ wa Langa kutoka katika lindi la mateso ya dawa za kulevya ulipatikana kuanzia Machi mwaka huu, baada ya familia yake kumpeleka kijana wao kwa tiba maalumu ya kuachana na matumizi ya `madudu’ hayo. Na kweli, elimu imemwingia na kujikuta akirejea ufahamu wake wa kawaida.

Ametangaza kuachana na `unga’, pombe, sigara na badala yake amejikita zaidi katika mazoezi ya kurudisha mwili wake katika hali ya kawaida. Aidha, amekata shauri la kuirudia fani yake na tayari ana vitu vipya, Bombokiata na Mteja Aliyepata Nafuu.

Anasisitiza kwamba, kutokana na mateso aliyoyapata, anakusudia katika siku za baadaye afungue kituo chake cha tiba ya dawa za kulevya ili aweze kuwaokoa vijana wengine wanaoangamia kutokana na matumizi ya dawa hizo haramu zinazopigwa vita karibu kote duniani. “Nimenusurika, namshukuru Mungu.

Nami najipanga kutaka kuwasaidia wengine waachane na mateso ya dawa za kulevya. Pia nichukue fursa hii kuwaomba msamaha wote niliowakosea kwa namna moja ama nyingine wakati nikiwa `teja’,” anasema Langa, kijana mwenye umri wa miaka 25.

Je, historia ya maisha ya Langa ikoje? Anasema Desemba mwaka 1985 jijini Dar es Salaam akiwa tunda la wanandoa Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo. Alisoma Shule ya Msingi Olympio na Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye Shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda. Baadaye alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma.

Huyo ndiye Langa Kileo msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye baada ya kulewa umaarufu na kujikita katika matumizi ya dawa za kulevya, ameibuka na kujutia `ujanja pori’, sasa akitaka kujiingiza katika kampeni ya kuwaokoa vijana wengine waliozama katika `unga’. Anakusudia pia kurudi darasani kujiendeleza na masomo ya elimu ya juu. Je, atafanikiwa? Kwa hakika, hili ni jambo la kusubiri na kuona. 
                                                          SOURCE JAMIIFORUMS

Wednesday 12 June 2013

Ney wa Mitego Awabeza Wasanii Wanao Mponda kwa Kupata Tuzo-Awaambia Atawatengenezea kiwanda na Kuwaajiri

  Rapper Ney wa Mitego, kupitia wimbo wa "Nasema nao" alifanikiwa kupata tuzo ya wimbo bora wa hiphop, ambao umesababisha malalamiko kwa baadhi ya wasanii wengine ambao wnaona hakustahili kuchukua tuzo hiyo kwa wimbo huo, huku wengine wakidai Fid q anastahili na wengine kudai Stamina ndio anastahili....leo hii Ney mwenyewe kafunga juu ya swala hilo
"aah wasanii ndio wanaolalamika na wameandika kwenye mitandao, lakini mwisho wa siku lazima tukubali matokeo kwamba mziki unabadilika kila kukicha, mi nawaambia wasanii wenzangu kwamba mkiendelea kung'ang'ania huko mtakufa njaa, halafu mwisho wa siku wataendelea kulia tu kila siku kwamba kuna hili mara lile,mi naimani kwamba mashabiki wangu ndio wamenikabidhi tuzo, media zinazosapoti kazi yangu ndio zimenisaidia mpaka mimi nimezungumza na mshabiki wangu popote walipo mpaka juzi nimepata tuzo ya wimbo bora wa hiphop. mi nastahili kupata tuzo, kwasababu kwanza sijui wao wanafanya hiphop gani, wakae waeleze mziki wao wao ni hiphop kwasababu hii na hii na hii na wangu sio hio hiphop kwasababu hii na hii na hii. bwana hiphop ni ukweli na unabadilika kila siku kila kukicha. Mi nawashauri tu kitu kimoja, sitaki kubishana na msanii yoyote, wana njaa, wakiendelea kung'ang'ania huko watakufa njaa, kwanini watu wamemsapoti Ney, kwanini watu wamemsapoti Kala Jeremiah,angalia mashairi ya Kala yako wazi, lakini we unaweka sijui mafumbo ya dizaini gani nani atakuelewa...........
halafu tuzo sio lazima upate tuzo, sio lazima ulaumu, kuna wasanii wakali hawajawahi kupata tuzo lakini hawajawahi kulalamika, kuna wasanii kama Juma Nature, nani anaweza kusimama stage na Nature? sijawahi kumsikia anaongea.....
category moja tu nimewekwa nimetusua wao wanalia, shauri yenu shauri yenu, jipangeni mwakani, mi staki kubishana nao, am the best, halafu wasipoangalia nawatengenezea kiwanda kwa ajili ya kuwaajiri wanapoendelea kuwana na hali ngumu, natengeneza kiwanda ambacho ntawaajiri wasanii  wanaofeli wote kwasababu hawana shughuli za kufanya." amesea Ney. Msikilize Hapa akiongea:

Tuesday 11 June 2013

RAIS KIKWETE AAPISHA MABAROZI WAWILI DODOMA


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakiwa na mabalozi wapya walioapishwa leo Juni 11, 2013 katika Ikulu Ndogo Dodoma. Mabalozi hao ni Mhe Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kuli) , anayekuwa balozi wa Tanzania nchini China na Mhe Anthony Cheche (kushoto) anayekuwa Balozi wa Tanzania katika Congo DRC.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Mhe Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kuli), anayekuwa balozi wa Tanzania nchini China.
sa5,4, 1:Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Mhe Anthony Cheche (kushoto) anayekuwa Balozi wa Tanzania katika Congo DRC.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu  na Makamu wa Rais DktbMohamed Gharib Bilal pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Makatibu wakuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Maskini Mrembo Achinjwa kama kuku na Kutupwa Jalalani Mikocheni B

MREMBO aliyejulikana kwa jina la Pepetua Maina au maarufu kama Lucy, Mkikuyu wa Kenya anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mpaka 30 amekutwa amekufa kwa kuchinjwa shingo na mwili wake kutupwa katika shimo la taka.
Mwili wa huo ulikutwa na polisi Juni 8, mwaka huu  Mikocheni B, jirani kabisa na makazi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
Kwa mujibu wa mtoa habari, mwili wa msichana huyo ulionekana na mfanyakazi mmoja wa ndani wakati akienda kutupa takataka eneo hilo ambapo alipouona alipiga kelele zilizowafanya majirani kukimbilia eneo la tukio na kujionea wenyewe.
Taarifa za kipolisi zilidai kuwa mrembo huyo kabla ya kuchinjwa alipigwa kwani mkono mmoja wa kushoto ulivunjika na kukutwa na jeraha kubwa katika paji la uso.
Wakizungumza na Uwazi kwa tahadhari kubwa kuogopa ushahidi, baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema hawakusikia vurugu zozote usiku kwa hiyo huenda wauaji walimchinja mbali na kwenda kuutupa mwili wake eneo hilo.

Juni 9, mwaka huu, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura kuhusu kifo cha msichana huyo ambapo alikiri kutokea.
Kamanda Wambura alisema kuwa, Pepetua alikuwa akifanya kazi kwa Jaji Engera Kileo kwa miaka mitatu mpaka siku ya kifo chake.
“Jeshi la polisi tulipokea habari za kuwepo kwa mwili huo jana (Jumamosi) saa sita na nusu, tukaenda na kuukuta ukiwa kwenye shimo la taka umechinjwa shingoni na kiganja cha kushoto kilikatwa na kitu chenye ncha kali na kwenye paji la uso alipasuliwa.
“Tuliuchukua na kwenda kuuhifadhi Hospitali ya Mwananyamala. Vijana wawili wanaoishi kwa Jaji Kileo ndiyo waliofika hospitali na kumtambua marehemu. Jaji mwenyewe alikuwa safarini nje ya nchi, amerejea leo (juzi Jumapili).

“Mpaka sasa tunamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano kuhusiana na kifo hicho, siwezi kuzungumza kwa undani zaidi,” alisema Afande Wambura.

YALIYOJILI BIG BROTHER AFRCA

Bolt na Betty wamekuwa Tight toka wameingia ndani ya nyumba hiyo siku ya kwanza , Wamekuwa Kishare Kitanda kimoja toka wameingia Big Brother...

SABABU NNE ZA OBAMA KUJA TANZANIA

 Marekani imetaja sababu nne ambazo zimemfanya Rais Barrack Obama kuijumuisha Tanzania katika ziara yake ya bara la Afrika.
Rais Obama amepanga kulitembelea bara la Afrika kuanzia Juni 26 hadi Julai 3, mwaka huu na atazitembelea pia Senegal na Afrika Kusini.
Kiongozi huyo wa Marekani ambaye baba yake mzazi ni mzaliwa wa Kenya, anatarajiwa kuwasili nchini Julai Mosi kwa ziara ya siku tatu. Atakuwa Rais wa tatu wa Marekani kuitembelea Tanzania baada ya Bill Clinton mwaka 2000 na George Bush mwaka 2008.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Balozi wa Marekani, Alfonso Lenhardt alisema sababu ya kwanza ya Obama kuja Tanzania ni kutokana na kuwa mfano wa utawala bora, demokrasia na ushirikishaji wa watu wake wakati wa kufanya uamuzi unaogusa maisha yao ya kila siku.
Alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano linapokuja suala la uongozi bora na ndiyo maana imekuwa na amani na utulivu kwa muda mrefu ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
“Nchi nyingi za Afrika zinazoizunguka Tanzania zimekuwa na matatizo ya vita vya wenyewe na hata ukosefu wa utawala bora,” alisema Balozi Lenhardt ingawa alidokeza kuwa katika siku za karibuni imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na matukio ya uvunjifu wa amani.
Balozi Lenhardt alisema sababu nyingine inayomfanya Rais Obama kuja Tanzania ni kutokana na jitihada za Serikali ya Marekani kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na kasi ya ukuaji wa uchumi.
“Rais Obama anakuja kuunga mkono juhudi za Watanzania katika kutengeneza mazuri ya uwekezaji lakini bila kusahau kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania imeivutia Serikali ya Marekani,” alisema.
Balozi Lenhardt alitaja sababu nyingine inayomleta Rais Obama kuwa ni kuisaidia Tanzania kuendeleza fursa mbalimbali za kujiletea maendeleo.
Alisema uendelezaji huo wa fursa una lengo la kuisaidia Serikali ya Tanzania kukabiliana na tatizo la umaskini.
Alisema Marekani ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kutoa fedha nyingi za misaada na akisema kwa mfano, mwaka 2012 pekee ilitoa Dola 750 milioni.
Aidha, alisema nchi yake imekuwa ikitoa misaada mingi kupitia Shirika la Millenium Challenge (MCC), ambayo imejikita zaidi katika kusaidia sekta za umeme, maji na miundombinu.

Alisema Tanzania inaunga mkono jitihada za Serikali kujitosheleza kwa chakula na inafadhili Mkakati wa Kukuza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).
“Tunaunga mkono mpango wa SAGCOT kupitia Mfuko wa Rais wa Marekani unaoitwa `Feed the Future’ lengo likiwa kuifanya Tanzania kupiga hatua katika kilimo,” alisema balozi huyo.
Sababu nyingine ya ujio wa Obama ni kuhimiza haja ya Afrika kutayarisha viongozi wa kizazi kijacho. Ameanzisha programu ya kuandaa viongozi wa kizazi inayoitwa `Young African Leaders Initiative’ na Watanzania watatu, Modesta Lilian Mahiga, Masoud Salim Mohamed na Malula Hassan Nkanyemka walishiriki katika mpango huo na kukutana na kiongozi huyo mwaka 2010.
“Rais Obama anataka kusaidia kuandaa viongozi wa kizazi kijacho wa Afrika kusimamia vizuri rasilimali za nchi,” alisema.
Tishio la China
Akizungumzia ushindani na China kuhusiana na fursa za kuwekeza na kuvuna rasilimali za Afrika, Balozi Leinhardt alisema hawana tatizo lolote na hilo kwani dhamira ya Marekani ni kusaidia Tanzania kupiga hatua katika maendeleo ya kiuchumi.
Rais wa China, Xi Jinping aliitembelea Tanzania Machi mwaka huu na ujio wa Obama umetafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni ushindani wa mataifa hayo mawili katika kusaka na kunufaika na rasilimali za Afrika.
Balozi Lenhardt alieleza imani yao ni kuwa China inadumisha urafiki na Tanzania kwa nia ya kuisaidia kuendelea... “Sisi hatuna shida na China, kwani tunaamini wako kwa ajili ya kusaidia. Ilimradi tu wawe na dhamira safi katika kuwasaidia.”
Alipoulizwa kama ziara ya Rais Obama ina lengo la kusaka fursa ya kuvuna rasilimali za Tanzania, balozi huyo aliwataka Watanzania kuacha kuwa na wasiwasi wa kuporwa rasilimali zao.
“Watanzania ni watu wapole na wakarimu ila mna tatizo moja la kuhofia kila jambo. Kila kitu mnachofanyiwa mnaona kuna baya linakuja. Sisi tuna nia njema ya kuwasaidia kuendelea.”

HATIMAYE WILFRED LWAKATARE APATA DHAMANA

Hatimaye Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Kamanda Wilfred Muganyizi Lwakatare 'Lwaks' leo apata dhamana na kurudi uraiani, baada ya Mahakama ya Kisutu kuamua kuwa dhamana yake iko wazi na sasa masharti tu ndiyo yanakamilishwa.
Lwakatare ameachiwa kwa dhamana ya Million 10

‘Madeni yameielemea Serikali’

Dodoma. Zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya Bajeti Kuu ya Serikali kusomwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge amesema Serikali imeelemewa na mzigo wa madeni.
Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa anatarajia kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2013/14 keshokutwa.
Chenge alisema hayo juzi Mjini Dodoma baada wa mkutano wa majadiliano ya namna bora ya utendaji kazi baina ya Kamati ya Bunge ya Bajeti na kamati za Miundombinu, Ulinzi na Usalama, Mambo ya Nje, Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
Alisema Serikali imeelemewa na madeni huku kila wizara ikitaka kukamilishiwa mafungu yake ya fedha jambo ambalo linashindikana kwa kuwa hazipo.
Kwa mujibu wa hotuba ya Kambi ya Upinzani ya Wizara ya Fedha, mpaka sasa deni la taifa limefikia Sh21.028 trilioni bila dhamana ya Serikali kwa mashirika ya umma na binafsi hadi kufikia Desemba 2012 na kati ya fedha hizo, asilimia 75.97 ni deni la nje.
Hata hivyo, katika majibu ya Serikali, Waziri Mgimwa alisema Serikali imeanza kulipa na kuanzia Julai 2012 hadi Aprili 2013, malipo ya madeni yamefikia Sh1,666.77 bilioni na kati ya hizo, deni la nje lililolipwa ni Sh213.57 bilioni.
“Unapoamua kuminya eneo moja kwa ajili ya kupeleka fedha eneo jingine, hapa panapominywa wanahangaika na wao wanahitaji fedha, inatakiwa kutafuta njia nyingine ya kupata fedha kwa ajili ya eneo hilo,” alisema Chenge.
Mwenyekiti huyo alisema wizara zote 32 zinahitaji fedha kulingana na bajeti wanazowasilisha bungeni wakati wizara nyingine zikihitaji fedha zaidi ili kukamilisha mipango kwa matumizi ya kawaida na maendeleo.
“Katika vikao vyetu vya ndani, tumezungumza na kila wizara. Zina matatizo mengi kweli... wanatutaka tuwaongezee kasma, sasa sisi siyo Serikali, tunachokifanya kamati ni kuishauri Serikali kuelekeza fedha eneo moja lenye mahitaji ya fedha nyingi kwa masilahi ya taifa.
“Tumeishauri Serikali kuondoa fedha maeneo kadhaa na kuitaka kutenga fedha kwa ajili ya mipango ya maendeleo, lakini wakati mwingine, hata hizo fedha zenyewe hakuna kwa kuwa tunachokitegemea zaidi hapa ni pato la ndani. “Sasa watu walipe kodi. Tabia ya ukwepaji kodi inasababisha Serikali kushindwa kukusanya mapato yake. Watu wanalalamika hakuna hiki na hiki, lakini wananchi na taasisi mbalimbali wenyewe ndiyo hao wanaokwepa kodi, sasa utapata wapi fedha za maendeleo?

Maalim Seif aikosoa Rasimu ya Katiba Mpya

Zanzibar. Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema hajaridhishwa na rasimu ya kwanza iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia maelfu ya wafuasi wa chama chake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Tundangaya Matemwe iliyoko Wilaya Kaskazini ”A’ Unguja.
Alisema chama chake kimeunda jopo la wanasheria weledi kwa lengo la kuipitia na kuichambua kifungu baada ya kifungu ili kutoa ushauri kuhusu rasimu hiyo.
“Rasimu hiyo mimi sikuridhika nayo tumeiona na tumeipitia na tumeunda jopo la wanasheria ili watushauri,” alisema Maalim Seif huku akishangiliwa na wanachama wake.
Alibainisha kuwa kuna mambo ambayo yalitakiwa yatolewe katika mambo ya Muungano ndani ya rasimu hiyo ambayo yangetoa mamlaka kamili ya Zanzibar bado yamebakishwa yakiwa ni mambo ya Muungano.
Mambo hayo ni kama ulinzi na usalama, sarafu na Benki Kuu, mambo ya nje ,usajili wa vyama vya siasa ushuru wa forodha na mapato yasio ya kodi yatokanayo na mambo ya muungano
Alisema kwa Zanzibar kwa yale mambo ambayo si ya Muungano wataweza kushirikiana na nchi yoyote ile duniani.
Alisema kuna baadhi ya mambo walitaka kuwamo ndani ya rasimu ya Katiba Mpya kuna baadhi ya mambo hayo yamo na mengine hayamo kabisa lakini mengine hayamo na mengine yamo nusu.
Hata hivo akizungumzia suala la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura alisema ili uweze kutoa uamuzi wa nchi yako lazima uwemo katika daftari la wapiga kura la Wazanzibari kama humo huwezi kupiga kura.
Alimtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jecha Bakari Jecha kuwa tume yake ni mpya tayari imepanga mikakati ya kuwakosesha wananchi kujiandikisha kwa kutumia mawakala au sheha akimkataa tu mtu basi asiandikishwe.

Tuesday 4 June 2013

TUME YA PINDA YAIBUA MADUDU ZAIDI ELIMU.

Dar es Salaam. Tume ya Kuchunguza Matokeo ya Kidato cha Nne iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda imebaini zaidiya matatizo 20 yanayozorotesha kiwango cha elimu na hata kusababisha maelfu ya wanafunzi kufeli mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Profesa Sifuni Mchome alisema inachunguza mfumo mzima wa elimu na kuwa suala la Matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2012 nimoja kati ya mambo wanayoyafanyia kazi. Mchome ameeleza hayo siku mojabaada ya gazeti dada la ‘The Citizen’ kuchapisha habari za kujiuzulu kwa mmoja wa Wajumbewa Tume hiyo, Rakesh Rajani aliyefikia uamuzi huo kutokana nakile alichosema ni kutoridhishwa na pendekezo la kufutwa kwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne. Alisema ripoti ya Tume hiyo itakayowasilishwa kwa Waziri Mkuu, Juni 15 mwaka huu, imebaini mambo mengi ikiwa ni pamoja na mitalaa kupitwa na wakati pia idadi ya wanafunzi kuwa kubwa na kuelemewa kwa mfumo wa elimu nchini. “Kuna mambo ya kuangalia ubora,kuna suala la ofisi na taasisi mbalimbali zinafanya kazi gani? Vipi uwajibikaji wake, majukumu yake na mgawanyo ukoje, Ofisi yaKamishna inahusika vipi na mitihani, huku kote tumeona kuna matatizo,” alisema. Alisema pia morali ya walimu imeshuka, jambo linalofanya wengikuwa tayari kuachana na kazi hiyo wakipata jambo jingine la kufanya. “Wengi morali imeshuka, wangepata nafasi ya kuchoropoka (kuondoka) wangekimbia, lugha ya kufundishia ni tatizo na mchango wa wazazi kwenye elimu ni wa kuangalia, yote haya ni matatizo,” alisema. Alisema kuna haja ya sera mpya ya elimu ambayo imekuwa ikizungumzwa tangu mwaka 2008 ili kutatua matatizo yaliyopo sasa. Akizungumzia kujiuzulu kwa Rajani, alisema sababu aliyotoa haina msingi kwani muda mwingi hakuweza kufanya kazi na tume hiyo. “Rajani ushiriki wake kwenye tume ni chini ya asilimia 10, muda mwingi alikuwa anasafiri au anakuwa kwenye kazi za asasi yake, mambo mengi alikuwa hajui na sisi tulikuwa kila kitu tunaamua kwenye vikao, kuna kazi tuliyompa ya kuangalia kamakila tulichojipangia kimefanyika kwa wakati, alishindwa kwa sababu muda mwingi hakuwapo,” alisema: Alisema kuwa, msimamo wa Rajaniulikuwa ni kuachana na wanafunziwaliofeli na badala yake tume ijikite kuangalia mambo mengine, jambo alilosema lilikataliwa na wajumbe wengine. “Sisi tuliona kuwa ni ukweli mfumouliotumika kupanga matokeo ulikuwa tofauti na kukaonekana kwamba ukibadilishwa matokeo yatakuwa tofauti, ndiyo maana tukasema matokeo yapangwe upya.

Wednesday 29 May 2013

The Tz: SIMU ZISIZO SAJILIWA KAAPUNI

The Tz: SIMU ZISIZO SAJILIWA KAAPUNI

PIGO KUBWA KWA MSANII WA TANZANIA KUPOTEZA MAISHA SOUTH AFRICA.

Ameandika Saico Dos KIFO CHA ALBERT MANGWAIR 28/May/2013, R.I.P!!! kiukwel alikuwa yeye na jamaa zake 3 yan walikuwa wa 4, Leo asubuh walikuwa wanarud Brixton wakitokea town Joburg na Ngwair tiketi yake ya ndege ilikuwa tayar kwa ajir yakusafir Leo hii hivyo tulikuwa tayar kumsindkiza Airport Leo Asubuh, hvyo wakamgongea mlango mshikaj akawafungulia, waliingia ndan lakn wakawa wapo kama tungi hivi, sasa ikawa wanaendelea kula mambo yao ndan, ila ghafla kama Mangwair akaanza kujisikia ovyo hv, then akaanguka nakujihs anapoteza faham watu wakaona kama anafanya masihala, so ikazd had mida ya saa sita mchana ikawa serious pia jamaa mwingine nae akapoteza faham hvyo hvyo coz walizidisha mambo kutumia, nas tukaitwa kumchek ikabd tuogope mpaka mida ya saa nane mchana ilibd tumpigie simu jamaa fulan Msouth Africa ni Taxi Driver ili tumpeleke Hospital coz sis tuliogopa kumpeleka na magar yetu Binafsi, akaja tulimchukua pamoja na yule mwingne had hospital kufika kule Doctor kumchek alikuwa tayar ameshakufa na yule mwingne bado yu hai ila hali yake sio nzur, ilibd jamaa Kat yetu aka sign kuhusiana na kufa kwa Albert Mangwair hvyo kesho Doctor atatupatia karatas ili tukabdhiwamwili wake kwa ajr yakuusafirishaTanzania!! Hivyo Ndvyo ilivyokuwa had kufa kwa Albert Mangwair mwili wake upo Helen Joseph Hospital in Hursthill next to Aukland park and University of Johannesburg, also Brixton and Westdene in Johannesburg South Africa!!

Saturday 25 May 2013

‘ASILIMIA 31 YA WATANZANIA NI WALEVI.'

Dodoma. Asilimia 26.8 hadi asilimia 31.9 ya Watanzania wanatumia pombe na asilimia 27.4 kati ya hao ambao ni wanaume na wengine asilimia 13.4 ambao ni wanawake, ni walevi wa kupindukia. Bunge lilielezwa jana. Takwimu hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, ambaye alisema kuwa viwango hivyo vimetokana na utafiti uliofanywa kati ya Februari hadi Oktoba mwaka jana 2012. Kwa mujibu wa naibu waziri, utafiti huo ulifanywa na Shirika laAfya Duniani (WHO). Alikuwa akijibu swali la Abdallah Haji Ali (Kiwani–CUF) aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu utumiaji wa pombe ambao umethibitika kuwa ni hatari kwa afya za binadamu. Pia alipendekeza pombe ipigwe marufuku kabisa hapa nchini kwa kuzingatia madhara yake. Naibu waziri alisema tafiti zimeonyesha kuwa watu milioni mbili wanafariki dunia kila mwaka duniani kutokana na madhara ya matumizi ya pombe na asilimia nneya matatizo ya kiafya yanatokana na matumizi ya pombe. “Hali inazidi kuwa mbaya zaidi katika nchi zinazoendelea hasa kutokana na kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi na ustawi wa jamii inayochangiwa na magonjwa ya malaria, kifua kikuu na Ukimwi,” alisema Dk Rashid. Naibu Waziri alisema kutokana na kuongezeka kwa athari zitokanazo na matumizi ya pombehasa kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Serikali inatekeleza mkakati wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukizwa unaoelekeza kutoa elimu kwa wananchi kupitia njia mbalimbali. Kuhusu mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo, alisema tayari Serikali imeanza utaratibu wa kuziwezesha hospitali za rufaa zamikoa, kuanza kutoa huduma kwawaathirika wa matumizi ya dawa za kulevya na pombe.

SAKATA LA GESI MTWARA: WABUNGE WA CCM WACHARUKA.

Dodoma. Wabunge wa CCM wamekuja juu na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi vigogo wa Serikali mkoani Mtwara, wakiwamo Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kutokana na kile walichoeleza ni uzembe uliochangia vurugu zinazoendelea za wananchi kugomea gesi kutoka nje ya mkoa huo. Wengine waliopendekezwa kuchukuliwa hatua ni kamati nzima ya ulinzi na usalama ya ngazi ya mkoa na wilaya ya Mtwara mjini, wakiwamo makamanda wa polisi. Kutokana na hali hiyo, vigogo kadhaa mkoani humo wako hatarini kukumbwa na ghadhabu hiyo akiwamo Mkuu wa vikosi vyaJeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mkuu wa mgambo na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Wabunge hao walikuwa wakitoa mapendekezo hayo kwenye kikaocha Kamati ya Wabunge wa CCM iliyofanya kikao cha dharura juzi usiku, mjini hapa. Kikao hicho kiliongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, huku Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye wakati huo alikuwa kwenye kikaocha Kamati ya Uongozi wa Bunge,aliwakilishwa na Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama. Katika kikao hicho maalumu kilichokusudia kutoa ushauri kwa Rais Kikwete juu ya njia mwafakaya kutatua hali ya machafuko, wabunge wengi wali kukasirishwa na jinsi hali ilivyo mkoani Mtwara. Chanzo chetu kwenye kikao hichokilieleza kuwa wabunge hao walichukizwa na jinsi Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya walivyokuwa wakipingana kimsimamo. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Joseph Simbakalila, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Wilman Ndile na Kamanda wa Polisi Mkoa Linus Sinzumwa wamehusishwa. Licha ya baadaye kuonekana kuwa kitu kimoja, wabunge hao walidai kuwa walishindwa kutumianafasi zao katika kutatua tatizo hilo, ambalo hadi juzi Serikali ilisema walikuwa wamekufa watu watano, wakiwamo wanajeshi wa JWTZ waliofariki katika ajali wakati wakienda kutuliza machafuko. Chanzo hicho kilieleza kuwa iwapomapendekezo ya wabunge hao yatapelekwa kwa Rais Kikwete kama michango ya wabunge hao ilivyokuwa, huenda rungu likawaangukia pia viongozi wa kisiasa wa CCM mkoani humo. Miongoni mwa wanasiasa hao, chanzo hicho kimesema ni wale waliotoa kauli za waziwazi kuungamkono msimamo wa kutoruhusu gesi kusafirishwa nje ya mkoa huo. “Hapa wapo wabunge, madiwani na viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM,” kilieleza chanzo hicho. Hata hivyo, baadhi ya wabunge walipendekeza mkakati wa kutatua uzembe uliofanyika Mtwara, unapaswa kuchukuliwa kwa uangalifu usije ukasababisha madhara mengine kwa Chama na Serikali. Walisema suala hilo halina budi kuchukuliwa kwa uangalifu hasa ikizingatiwa kuwa Chama cha CUF ndicho chenye nguvu mkoani humo ukilinganisha na vyama vingine vya upinzani. Wabunge hao walikituhumu chamahicho kuwa kimekuwa kikijaribu kutumia vurugu hizo kama kigezocha ushawishi wa kukubalika mkoani humo.