Thursday 9 May 2013

TANGAZO KUTOKA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA.

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA Kutokana na Chuo kufungwa, Baraza la Uongozi wa Chuo katika kikao chake cha dharura cha tarehe 03 Mei 2013 kimeagiza wanafunzi wote kuanziangazi ya Cheti mpaka Stashahada ya Uzamili kuzingatia yafuatayo: 1. Kila Mwanafunzi anatakiwa kutuma maombi mapya ya kujiunga na Chuo. 2. Barua ya maombi hayo ipitishwe kwa Mkuu wa Wilaya anapoishi mwanafunzi. Kwa mwanafunzi wa Stashahada ya Uzamili ya Uhasibu barua yake ya maombi ipitie kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali. 3. Katika maombi hayo mwanafunzi anaagizwa kueleza namna alivyoshiriki katika vurugu za tarehe 24 Aprili 2013. 4. Mwanafunzi awe amekamilisha malipo ya ada iliyobaki wakati anatuma maombi yake. 5. Mwisho wa maombi ni tarehe 16 Mei 2013. Maombi yapelekwe kwa anwani ifuatayo: Mkuu wa Chuo, Chuo cha Uhasibu Arusha S. L. P. 2798 Arusha. 08 Mei 2013 TEMBELEA TOVUTI YA CHUO www.iaa.ac.tz UPATE TAARIFA MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE.

USAJILI WATAHINIWA KIDATO CHA SITA 2014 KUANZA JULAI 2013

Baraza la Mitihani la Tanzania linawatangazia watu wote wanaotaka kufanya mtihani wa kidato cha sita (ACSEE) mwezi Mei 2014 kama watahiniwa wa kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kitaanza rasmi tarehe 1 Julai, 2013 kwa ada ta shilingi 35,000/= na kipindi cha bila malipo kitaisha tarehe 31 Ag o sti, 2013 . Kuanzia tarehe 1 Septemba, 2013 hadi tarehe 30 Septemba, 2013 waombaji watajisajili kwa ada ya shilingi 50,000/= (Ada pamoja na faini). Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti www.necta.go.tz ya Baraza la Mitihani la Tanzania. Kabla ya kujisajili kwenyemtandao, waombaji watapaswa kuchukua namba rejea (Reference number) katika vituo vya mitihani na watazitumia wakati wa kujisajili. Hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila n a mba rejea kutoka katika kituo anakotarajia kufanyia mtihani. Wakuu wote wa vituo nchini watakabidhiwa namba rejea kabla ya muda wa kujisajili kuanza na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo . IMETOLEWA NA KATIBU MTENDAJI BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA Baraza la Mitihani la Tanzania

WAYNE ROONEY AOMBA KUONDOKA OLD TRAFFORD

Uongozi wa United wameshikwa na butwaa kufuatia straika wakeWayne Rooney kuomba kuondoka klabuni hapo. masaa manne kabla Sir Alex Ferguson hajauthibitishi a uongozi wa juu wa klabu hiyo kuhusu kuachia ngazi kwake kama meneja wa United mwishoni mwa msimu huu, kumpisha meneja wa sasa wa klabu ya Everton David Moyes kushika hatamu, Sportsmail wametanabaisha kwamba Rooney alimwambia Ferguson wiki mbili zilizopita anataka kuanza upya. Kama Rooney atabakia klabuni hapo na Moyes kushika wadhifa huo utakaoachwa na Ferguson basi atapata fursa ya kufanya kazi tena na bosi wake wa kwanza Moyes - ambaye anatarajiwa kuthibitishwa muda wowote leo. Akiwa anakasirishwa na yanayomtokea hapo klabuni, Rooney na Ferguson wakiwa kwenye hicho kikao katika ofisi zameneja huyo kua ni bora aachwe aondoke pindi dirisha la usajili litakapofunguli wa mwezi wa saba. Taarifa zinaendelea kudai kwambaFerguson, alimwambia kwa kufuatia hawezi kumthibitishia kumuuza ama kutokumuuza. Rooney kwa sasa atafikiria upya kua chini ya kocha wake huyo wazamani Moyes, ingawa hapa kipindi cha nyuma wameshasemeana mbovu. Bado inasubiriwa kuona kwamba baada ya maongezi kama Rooney atashupalia suala hilo na kuiandika barua rasmi ya kutaka kuondoka klabuni hapo. Rooney anajua kwamba Chelsea wako tayari kumchukua muda wowote kujiuga Stamford Bridge, ilhali Bayern Munich na Paris Saint-Germain nao pia wangependa kufanya nae kazi. Haya kama shabiki wa Chelsea ungependa kumuona Rooney Stamford Bridge? Mpenzi a Man U - ungefurahia abaki ama aondoke tu. Kazi ni kwako mwanamichezo wa The Tz.

SAKATA LA KUFUTWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE LAINGIA DOSARI,NECTA WATANGAZA KUJIUZULU ENDAPO YATAFUTWA...!!

Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwe ­kaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne. Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukan ­dala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao. Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafa ­nya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala. Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo

Wednesday 8 May 2013

It's Official: Sir Alex Ferguson will step down as Manchester United manager at the end of the season after 26 years in charge. The Scot, 71, has won 38 trophies since taking over from Ron Atkinson on 6 November 1986, including this season's Premier League title.

GADNER G HABASH (MUME WA JAYDEE) AKAZIA WOSIA WA J...

Tumanyene: GADNER G HABASH (MUME WA JAYDEE) AKAZIA WOSIA WA J...: Gadner G Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki maarufu nchin Lady Jay Dee, amezungumza juu ya maneno aliyoyasema Lady Jay Dee ...

Tuesday 7 May 2013

(TAMKO LA BAKWATA) TAARIFA KWAVYOMBO VYA HABARI TAMKO LA BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA BAKWATA JUU YA MLIPUKO WA BOMU - ARUSHA

Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh. ... Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA, limepokea kwamasikitiko makubwa tukio la kurushwa bomu Kanisani na kusababisha upotevu wa maisha na majeraha kwa watu wengi wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo la Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Orasiti, Arusha. Kimsingi hili ni jambo la kusikitisha,kukera na kufadhaisha sana kutokea hapa nchini. Watanzania kwa miaka mingi, tumezoea hali ya utulivu na amani na tukio kama hili ni changamoto kwa usalama wa Watanzania wote nchinzima Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA linalaani kitendo hicho cha kikatili na inaviomba vyombo vya dola kufanya jitihada zote kuhakikishawahusika wanakamatwa na wanachukuliwa hatua, kwani msiba huu ni wetu sote, Wakristo na Watanzania wote. Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania mimi SheikhIssa Bin Shaaban Simba Mufti wa Tanzania nawapa pole wafiwa wote katika tukio hilo na kuwaombea dua majeruhi na Mwenyezi Mungu (SW) awape tahfif na wapone haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku. Wabillahi Tawfiiq. SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA. MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA BARA.

SAKATA LA BOMU ARUSHA

FBI watua nchini, EU wadai Udini ni chanzo, ukomeshwe Dodoma/Arusha. Wakati maofisa wa Shirika la Upelelezi wa Marekani (FBI) wametua Arusha, raia wanne wa Saudi Arabia na Watanzania wawili wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika kulipua bomu lililoua watu wawili na kujeruhi wengine 61 wakati wa ufunguzi wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Olasiti. Waliofariki dunia ni Regina Longino Kurusei (45), mkazi wa Olasiti na James Gabriel (16), ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana. Tukio hilo lilitokea wakati Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini, Francisco Montecillo Padilla alipokuwa akizindua kanisa hilo. Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alisema raia hao wa Saudi Arabia walikamatwa jana asubuhi baada ya tukio wakiwa kwenye gari wakielekea Kenya kupitia Namanga. Mulongo alisema raia hao wa kigeni waliingia nchini Jumamosi iliyopita na siku iliyofuata ndipo kukatokea ulipuaji huo. Alisema lengo la shambulizi hilo lilikuwa kumdhuru Askofu Padilla. “Mtu ambaye tulimkamata jana (juzi Jumapili) ndiye aliyesaidia kuwapata watu hawa wa Saudi Arabia na Watanzania hao,” alisema Mulongo. Mulongo alisema maofisa wa FBI walifika jana saa tano asubuhi ili kusaidiana na Polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika uchunguzi wa tukio hilo. Maofisa hao wa FBI walikuwa Zanzibar ambako walikuwa wanachunguza kifo cha Padri Evaristus Mushi ambaye aliuawa Februari 17, mwaka huu. Hii itakuwa mara ya pili kwa wageni kuhusishwa na matukio ya ugaidi nchini baada ya mwaka 1998 wakati raia kadhaa wa Misri wakiongozwa Fazul Abdulla waliposhirikiana na Watanzania kadhaa akiwamo Ahmed Ghailani kulipua ubalozi wa Marekani nchini na ule wa Kenya. Ghailani anatumikia kifungo cha maisha nchini Marekani wakati Fazul aliuawa Somalia mwaka 2011. Tamko la Serikali Akitoa tamko la Serikali bungeni jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alimtaja mmoja wa watuhumiwa wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo kuwa ni Victor Calisti Ambrose (20), mkazi wa Kwa Mrombo Arusha ambaye ni dereva wa bodaboda. Alisema kijana huyo ndiye anayetuhumiwa kurusha bomu hilo. Waziri Nchimbi alitoa onyo kali kwa wanasiasa wanaopandikiza chuki za kidini miongoni mwa Watanzania na kuishutumu Serikali kutokana na matukio kama hayo. “Kuna wanasiasa ambao wanaona masilahi yao ni muhimu kuliko maisha ya Watanzania, masilahi yao ni muhimu kuliko utulivu wa Watanzania na masilahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania.” JK akatiza ziara, Bilal atoa ahadi Rais Jakaya Kikwete, amekatiza ziara yake ya kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na shambulio la bomu kwenye kanisa hilo. Taarifa ya Ikulu imesema jana kwamba Rais Kikwete amelazimika kukatiza ziara hiyo na kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi. Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal ameahidi kuwa Serikali itahakikisha wote waliohusika na tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola. Balozi wa Papa atoa tamko Askofu Padilla ambaye jana alitembelea majeruhi katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru, alieleza kustushwa na tukio hilo na kusema hakutarajia kitu kama hicho kutokea wakati wa shughuli hiyo wakati Watanzania wakijulikana ni watu wa amani. Alilaani tukio hilo na kuvitaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli. Kanisa Katoliki Arusha Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Arusha jana liliitaka Serikali iwataje waliohusika na tukio hilo la kigaidi huku likiwataka waumini wake kutolipiza kisasi. “Msimamo wa kanisa katika hili, ni kuwataka waumini wasilipize kisasi kama ambavyo alisema Yesu Kristo kuwa msilipize kisasi, muwe tayari kushinda ubaya kwa wema,” alisema Askofu Josephat Lebulu na kuongeza: EU Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), imetaka kuharakishwa kwa uchunguzi wa tukio hilo na kuonya kuwa matukio kama hayo yanaweza kulitumbukiza taifa kwenye machafuko. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Balozi wa Umoja huo nchini, Filiberto Ceriani-Sebregondi alisema Tanzania inapaswa kufahamu kwamba pasipo kujenga, kuendeleza na kusisitiza utamaduni wa kuvumiliana, hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa siku za usoni.

MTUHUMIWA WA KURUSHA BOM ARUSHA AKAMATWA

Aliyerusha bomu Arusha akamatwa: DEREVA wa pikipiki maarufu kama bodaboda, Victor Ambrose, anatuhumiwa kurusha bomu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti jijini Arusha, lililosababisha vifo vya watu wawilina wengine karibu 70 kujeruhiwa.

Monday 6 May 2013

Soma Hapa Alichozungumza Ruge Mutahaba Juu Ya Lady Jay Dee Na Msimamo Wa Clouds

Haya ni mazungumzo ya Ruge Mutahaba na msimamo wa Clouds juu ya mwanamuziki Lady Jay Dee, mazungumzo ambayo yalifanyika kupitia kipindi cha Clouds fm cha cha Power Breakfast , mbali na mengi aliyoyaongea haya ni machache kti ya mengi na hivi ndivyo alianza: RUGE: As a country we need to discuss issue kwa maendeleo ya nchi, tuachane na ku-discuss ishu hizi kama personal issue. Ni kweli kwamba tulikuwa hatutaki kulizungumzia hili na hata sasa, ila kutokana na msukumo ladba ni vizuri kuliongelea, ila uamuzi ulikuwa ni wetu kama tuongee au tusiongee. Sometimes unahisi unahitaji kusikia upande wa pili, kwa binadamu yoyote, kwa maana kuna watu ambao wanaishi mbali na hapa mjini kama Kigoma nao wanapenda kujua juu ya swala hili kwa upande wa pili likoje. Ila tu niseme ni tatizo la mtu binafsi halina sababu ya kujadiliwa na kufanywa kama ni suala la kitaifa, sababu sura inayowekwa ni kama kitu kikubwa sana, binafsi bado sijajua nini hasa tatizo la kinachojadiliwa. Ikumbukwe kwamba Clouds ni chombo binafsi, ni chombo ambacho kilianzishwa kwa kufata sheria zote, na sisi tulichagua namna sisi tukavyoendesha redio yetu. Kama biashara yoyote na sisi tunafanya biashara kutokana na mipango yetu, na ndio maana kwa kipindi cha miaka 10 tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Hakua anayefanya sawa duniani akakosa kulaumiwa, sisi ni binadamu na tuna makosa ya kibinadamu kama binadamu wa kawaida. Nakumbuka ilikuwa ni tarehe 14-12 siku ambayo Lady Jay Dee kwa mara ya kwanza alipoandika kwenye mitandao ya kijamii ujumbe uliosema “ukinikosea nitakusimamisha na sitokuamsha tena”, Niliambiwa na jamaa wa Bongo5 na nikaamua kumpigia simu JD siku hiyo na nikamwambia kwamba, kuna maneno nimeambiwa kwamba wewe umeandika, yeye akasema hapana, namini nikamwambia sikiliza nikwambie kwa ninavyokwambia wewe , haya mambo hayafai. Baada ya kukata simu dk 10 akanitumia sms mfululizo, ya kwanza aliandika “Nililipa matangazo yangu ya laki 2 na 70, nimeambiwa kwamba umekataza yasipigwe. Sms nyingine ilisema “unaruhusu watangazaji wako wanitukane na kui-promote bendi yako ya Skylite”. Huku akiendelea Ruge akasema, unajua kwamba sisi biashara yetu ni matangazo, kwa nini nikatae, mbona siku zote tunayarusha matangazo yao? Na Gadna kila siku anakuwepo hapa kufanya matangazo? Ni swala la yeye kupita tu chini ni kuuliza kama kweli matangazo hayarushwi. Na kitu kingine ni kwamba, sio kweli na siwezi kumruhusu mtangazaji yeyote amtukane redioni. Mimi ishu ya skylite, Skylite wanalipa matangazo kama wateja na bendi nyingine zinavyolipia, na huwa tunawapa bonsai kama ambavyo huwa tunampa yeye JD. Nilimwambia JD angalia maana ni kweli kwamba Skylite wanakuja juu aangalie, hakika kuna upotoshwaji Skylite kuhusishwa Clouds, Skylite ni ya Sebastian Ndege, yeye analipa matangazo kama wengine wanavyolipa, akilipa laki 2 tunampa matangazo ya laki mbili kama bonasi. Skylite ilichukua wanamuziki watatu wa Machozi Bendi, kama ambavyo ilifanya kwa bendi Banana na TID. Kiukweli wakati haya yanaendelea mimi nilikuwa safari niliporudi baada ya hiyo tarehe 14,nikaona mbona hakuna jambo la kuzungumza au kujadili, katika yote ni nini anacholalamika hasa? Mbona sioni tatizo? Ishu ya kusema kwamba nyimbo zake hazipigwi, unajua hapa kwetu kuna systeme ambayo inaweza kuangalia na kujua wimbo katika muda flani ulichezwa mara ngapi, kupitia systeme hiyo tuliangalia na kuona kwamba wimbo wake wa Joto Hasira ulichezwa mara 46 mpaka siku tunasema hatupigi nyimbo zake. Tarehe 12-02 niliongea na Gadna na sio Jd juu ya kwenda kuazima stuli kwa ajili ya shooting, na tukazitumia na kisha tulizirudisha. Ni kweli kwamba tulikaa kikao binafsi sikuona kama kuna haja ya kutopiga nyimbo za JD, baada ya kutuma sms ya kwamba sisi tunaogopa ndipo tukasema Redio ina policy kwa utaratibu wetu, kwa anayetutukana, kutukebehi au maneno yoyot, basi nasi tutatumia njia zetu, na mpaka mtu huyo aje kwetu na tuongee na ku-apologize. Mbona Diamond nyimbo zake hazipigwi Magic fm mwezi wa saba sasa, kuna kipindi Fulani East Afrika walikuwa hawazipigi nyimbo za Ray C na pia za Alikiba. Sikuwahi kuona kwa nini jambo hilo kufanywa la kitaifa. Kuna Redio 82 hapa nchini, na mtu anapokwambia achane kupiga nyimbo yangu, kwa maana asipotaka yeye mwenye kwa kauli yake tusipige nyimbo yake, basi tunacha. Ni utaratibu tu…. Sioni tatizo la wananchi kulifanya jambo hili kama la kitaifa, kuna fulsa ya kujadili mambo mengi, kama ingekuwa mtu wa kugalagala chini kwa kuchukuliwa wanamuziki basi angekuwa ni Asha Baraka, ila ila kila siku kwa zaidi ya miaka 10 sasa anaamka anasimama, ndivyo ambavyo Lady Jay Dee anapaswa kufanya. Historia ya JD ni ndefu, kwa mara ya kwanza nilimsikiliza kwenye Redio yetu kupitia kipindi cha Taji liundi cha Apex, alikwa studio anarap, nikamwambia Taji nahitaji kesho aje ofisini, nilipoongea nae nikampa kazi ya kutangaza, alikaa kwa kipindi cha mwaka mzima bila kuimba, mara ya kwanza kumuweke ilikuwa ni kwenye wimbo wa Baba wa Taifa mwaka 99. Nikasema huyu mtu ni msanii mzuri na aanze kuimba, tulirekodi kwa Mika Mwamba na kwa msaada wa Mzee Muta. Sisi tukanzisha project ya Smooth Vibe yenye lengo la kuwajenga wasanii, kisha tukawambia mziki ni full time job na tuliwauliza je mnachagua kuimba au utangazaji? Lady Jd na Ray C wakachagua kuimba na Fina akaamua kuendelea na utangazaji. Ilipofika miaka mitano na tulipoona project imekwenda vizu tukaseama tuiache , tukaachana na project hiyo na yeye aaendelea zake. Kinachotuhuzunisha ni kwamba yeye ni kioo cha wasanii wachanga ambao wanatakiwa kuiga mfano wake kwa yale mazuri, na hapa ndipo penye taizo ambalo ni kuachiana kijiti, tatizo ambalo ni kubwa kwa wanamuziki wengi kujiandaa. JD anatakiwa ajitahidi kutengeneza uwazi kwa watu wajaribu kuelewa, sisi ni watu kama yeye, anashindwa basi atafute watu, na kama kuna tatizo la kitaasisi, mimi nipo wazi tayari kukutanana naye na kutafuta muafaka juu ya hili. Mtu kama Lady Jay Dee anapaswa kufikisha malalamiko yake kwa sehemu husika huku akiwa na vielelezo ili tuone muafaka wake. Ni vyema kuwaandaa wasanii wetu na wao wajiandae, naamini bado mda upo kwake yeye, cha msingi ni kwa yeye kurudi na kulisoma soko. Swala la Clouds kwamba inataka kuuwa muziki wa bongo fleva kwa makusudi, Clouds inategemea muziki wa bongo fleva kama mahudhui ya kipindi. Clouds kila weekend ndio Redio peke yake inayotoa udhamini kwa wasanii kufanya show zao Maisha na Bilicanas. Tamasha letu tunalofanya pekee ni Fiesta ndani ya miezi miwili kwa mwaka, hii ina maana kwa miezi mingine 10 wasanii huwa wanafanya show zao zaidi yah ii ya kwetu. Swala kwamba tulitaka kumpa laki nane akakataa, ni swalala makubaliano, ni kama vile mbavyo unweza kumpa msanii million mbili akakataa au mwengine ukampa laki sita akakubali, ni swala la makubaliano tu na ndivyo biashara hii na nyingineyo kwa vile ilivyo Ni kama yeye aliposhindwana Linah na Barnaba sababu ya kiwango cha hela ambacho alitaka kuwapa. Mimi nafikiri, JD inabidi akaze buti, anapigana wrong war, Skylite inamsumbua na akubaliane na ukweli kwamba hilo ndilo tatizo lake. Sielewi connection ya Nyumbani Lounge kwa Clouds na Ruge, binafsi nintachojua vita zake azielekeze kwa Skylite Bend na inabidi azielekeze huko, na aangalie tatizo lilitotokea Nyumbani Lounge naamini hiyo ndiyo sababu kuu. Cha msingi atafute mtu mwenye busara aangalie hili jambo hili litaishaje. Kwa kumalizia, hii nchi sasa na vyombo vinavyohusika inabidi virudi na kufanya kazi zake ipasavyo kwa mambo mbalimbali yanayotokea kwenye mitandao. Swala la kulaumiana halitatukuza, sisi ni Redio binafsi na tutafanya kile tunachotakiwa kufanya kwa matakwa ya walio wengi, chochote kinachotokea katikati. Hii ni redio binafsi na sisi tuna taratibu zetu, kama ambavyo tuliwa kupiga nyimbo za wanawake kwa siku nzima basi na kuanzia sasa leo tusipige bongo fleva. Msimamo wa kampuni, hili jambo hili hatutalizungumza, ila tunamtakia kila la heri kwenye show yake ya tarehe 31, ila atakapokuwa tayari kuendelea kufanya biashara na saisi katika zile redio 82 tutakuwa tayari kufanya kazi naye.
TAARIFA KAMILI KUHUSU MABOMU ARUSHA Waliojeruhiwa jumla ni 66, mtu mmoja amefariki (mwanakwaya) na kijana mwingine anashikiliwa naPolisi kama mshukiwa wa mlipuko huo...inadaiwa alikutwa na stock byingine ya mabomu alipokamatwa!! Waaliojeruhiwa ni pamoja na Consensia Mbaga(53) Christopher Raymond (10),Deborah Joachim(24) Elizabeth Isdori(24),Anna ­ Didas(52), Bertha Cosinery(49),Ed ­da Ndowo(77) ,Derick Cyprian(8),Faus ­tine Andrea (35),Mary okech,Neema Daud(13). Watu wengine ni Mesoit Siriri (33) ,Clenes pius(22),Joyce yohana (15) ,Restuta Alex(50), Mathias Riha (74), Magreth Andrew(45), James Gabriel (16), Regina James (17), Elizabeth Masawe(15), Elizabeth Sauli(18), Njau (35),Yasinta Msafiri (160 na Doreen Pancras(28). Idadi wajeruhi wengine ni Alex Arnold,Agripina ­ Alex(9),James Gabriel(16),lov ­eness nelson (17) ,Amalone Pius(25),Frank Donatus (10) ,Alphonce Nyalandu (26),Athanasia Reginald (14),Phillemon Ceressa(49) ,Neema Daud(13)Sophia Kanda(72) ,Theofrida Inocent(21), na Regina Darnes(17).

Sunday 5 May 2013

HAWA NDIO WACHEZAJI KUMI BORA KWA SASA DUNIANI.

10. Robert Lewandowski | Borussia Dortmund 9. Gareth Bale | Tottenham Hotspur 8. Zlatan Ibrahimovic | Paris St.Germain 7. Franck Ribery | Bayern Munich 6. Radamel Falcao | Atletico Madrid 5. Xavi | Barcelona 4. Robin Van Persie | Manchester United 3. Andres Iniesta | Barcelona 2. Cristiano Ronaldo | Real Madrid 1. Lionel Messi | Barcelona

WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa. Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari. Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki. Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa. Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao. Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria. Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu. Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia. Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa. Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao. Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni. Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu. Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame Enyi mtakaokuwa hai baada yangu. Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu. Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia. Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge. Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka. Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia.. Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star.. Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??. Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu. Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili. Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri. Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi?? Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa

Tisa wanaswa kwa kumkata mkono albino

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwarwanda alisema watuhumiwa hao walikuwa wakisakwa kwa muda mrefu kutokana na mtandao mkubwa waliokuwa nao, hatimaye baadhi wamefanikiwa kukamatwa huku wengine bado wakiendelea kutafutwa. Sumbawanga. Polisi katika Mkoa wa Rukwa likishirikiana na Polisi wa Tabora pamoja na kikosi kazi maalumu cha kitaifa, limefanikiwa kuwatia nguvuni watu tisa waliokuwa wakisakwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za kumkata mkono, Mwigulu Matonange(10) mlemavu wa ngozi Februari 15 mwaka huu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwarwanda alisema watuhumiwa hao walikuwa wakisakwa kwa muda mrefu kutokana na mtandao mkubwa waliokuwa nao, hatimaye baadhi wamefanikiwa kukamatwa huku wengine bado wakiendelea kutafutwa. Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Weda Mashilimu(29),Nickon Kadogoo(25), Peter Msabato(32),Ignas Sungura(27),Faraja Mwezimpya (31) pamoja na Kurwa Hamis (29) wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji ha Ilemba Rukwa. Aliwataja watuhumiwa wengine ambao ni Hamis Mnywanywa ambaye ni mganga wa jadi na mkazi wa Karema Katavi,James Paskali(24) mkazi wa majimoto, pamoja na Ibrahimu Tella(27) mkazi wa kijiji Masanula-Usule Shinyanga. Kamanda alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulifuatia uchunguzi wa kina uliokua unafanywa na polisi hao kupitia mawasiliano ya simu na taarifa mbalimbali za kipelelezi ambapo siku ya April 22 walifanikiwa kumnasa Nickon Kadogoo akiwa Katavi na mkono huo akiupeleka mkoani Tabora ambapo angepata soko. Baada ya kuhojiwa mtuhumiwa huyo alidai kuwa yeye na wenzake hao waliagizwa mkono huo na mganga wa jadi aitwaye Rashid Manywanywa, ambapo aliwaahidi angemlipa kila mmoja Sh600 milioni kama wangempelekea mkono huo. Alisema baada ya tukio la kumkata mtoto huyo mkono na kumpelekea mganga huyo alidai kuwa hana fedha zote hizo kwani wao walishindwa kutumia akili kwa kuwa hata yeye ni maskini angelipata wapi fedha zote hizo, hivyo hawezi kununua mkono huo. Baada ya kuona soko limeshindikana ndipo walipoamua kufanya mawasiliano na watu wengine na kuhakikishiwa katika Mikoa ya Tabora na Shinyanga kuna soko la uhakika ndipo safari ya kuelekea huko ikaanza. Kwa upande wake, mganga huyo wa jadi alikiri kuwaagiza watuhumiwa hao mkono huo na kudai kuwa alitaka kutumia kutengenezea chombo cha usafiri ambacho alidai kuwa ni ungo ambao unatumika na wachawi kusafiria nyakati za usiku. Kamanda huyo alisema watuhumiwa wote kutoka mikoa hiyo wamekamatwa na polisi na bado upelelezi unaendelea mara baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani wakati wowote.
Dodoma/Dar. Serikali imechukua uamuzi mgumu na kuamua kuwafariji wanafunzi waliofeli mitihani ya kuhitimu kidato cha nne mwaka 2012 baada ya kufuta matokeo hayo na kuamua yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011.
Uamuzi huo wa Serikali umetokana na matokeo mabaya ya mitihani huo yaliyosababisha zaidi ya asilimia 60 ya wanafunzi kupata sifuri.
Kutokana na matokeo hayo, Serikali iliunda Tume inayoongozwa na Profesa Sifuni Mchome kuchunguza matokeo hayo ili kupata ufumbuzi wa kudumu.
Muda mfupi baada ya tamko la Serikali, baadhi ya wadau wa elimu wameeleza kufurahishwa na uamuzi huo, huku Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kikiikosoa hatua hiyo, kuwa imekiuka sheria na kupora madaraka ya Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).
Akitoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu taarifa ya awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Matokeo ya Mtihani wa Taifa Kidato cha nne mwaka 2012 jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema wameagiza Necta kuweka viwango ili matokeo ya wanafunzi yalingane na juhudi zao.
“Standardization ifanyike ili matokeo ya wanafunzi yalingane na juhudi wazizoziweka katika kusoma kwa mazingira, hali halisi ya Tanzania na uamuzi wa taifa kuongeza idadi ya shule na wanafunzi wakati uwekezaji katika ubora unaendelea,” alisema Lukuvi.
Lukuvi alisema Necta imeelekezwa kuwa licha ya sheria ya kuanzishwa kwake kuruhusu kufanya marekebisho ya mchakato wa mtihani, marekebisho yoyote ya kubadilisha utaratibu wa kupanga viwango vya ufaulu na madaraja ya mitihani yanatakiwa yahusishe wadau wote wanaohusika na mitalaa, ufundishaji na mtihani.
“Wakati Tume inaendelea kukamilisha kazi yake, uamuzi wa Necta kutumia utaratibu mpya wa kupanga viwango vya ufaulu na madaraja ya matokeo ya mitihani uliotumika 2012 usitishwe,” alisema Lukuvi na kuongeza:
“Badala yake Necta itumie utaratibu uliotumika mwaka 2011 kwa kidato cha nne na sita kwa mitihani yote, ikiwamo utaratibu wa Standardization na kutoa matokeo mapya kwa kuzingatia maelekezo haya.”
Pia, Serikalli imeagiza mchakato wa tuzo wa taifa (National Qualifications Framework) na Mfumo wa Kutahiniwa/ kuthamini maendeleo ya mwanafunzi masomo yake (National Assessment Framework) ukamilishwe haraka iwezekanavyo.
Katika mtihani wa mwaka 2012, wanafunzi 367,756 walifanya mtihani huo na waliofaulu ni 126,847. Waliofaulu kwa kwa madaraja ya kwanza hadi la tatu ni 23,520 sawa na asilimia 6.4 na daraja la nne ni 103,327 sawa na asilimia 28.1, huku 240,909 ambao ni asilimia 65.5 wakipata daraja sifuri.
Kauli ya CWT