Tuesday 4 June 2013

TUME YA PINDA YAIBUA MADUDU ZAIDI ELIMU.

Dar es Salaam. Tume ya Kuchunguza Matokeo ya Kidato cha Nne iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda imebaini zaidiya matatizo 20 yanayozorotesha kiwango cha elimu na hata kusababisha maelfu ya wanafunzi kufeli mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Profesa Sifuni Mchome alisema inachunguza mfumo mzima wa elimu na kuwa suala la Matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2012 nimoja kati ya mambo wanayoyafanyia kazi. Mchome ameeleza hayo siku mojabaada ya gazeti dada la ‘The Citizen’ kuchapisha habari za kujiuzulu kwa mmoja wa Wajumbewa Tume hiyo, Rakesh Rajani aliyefikia uamuzi huo kutokana nakile alichosema ni kutoridhishwa na pendekezo la kufutwa kwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne. Alisema ripoti ya Tume hiyo itakayowasilishwa kwa Waziri Mkuu, Juni 15 mwaka huu, imebaini mambo mengi ikiwa ni pamoja na mitalaa kupitwa na wakati pia idadi ya wanafunzi kuwa kubwa na kuelemewa kwa mfumo wa elimu nchini. “Kuna mambo ya kuangalia ubora,kuna suala la ofisi na taasisi mbalimbali zinafanya kazi gani? Vipi uwajibikaji wake, majukumu yake na mgawanyo ukoje, Ofisi yaKamishna inahusika vipi na mitihani, huku kote tumeona kuna matatizo,” alisema. Alisema pia morali ya walimu imeshuka, jambo linalofanya wengikuwa tayari kuachana na kazi hiyo wakipata jambo jingine la kufanya. “Wengi morali imeshuka, wangepata nafasi ya kuchoropoka (kuondoka) wangekimbia, lugha ya kufundishia ni tatizo na mchango wa wazazi kwenye elimu ni wa kuangalia, yote haya ni matatizo,” alisema. Alisema kuna haja ya sera mpya ya elimu ambayo imekuwa ikizungumzwa tangu mwaka 2008 ili kutatua matatizo yaliyopo sasa. Akizungumzia kujiuzulu kwa Rajani, alisema sababu aliyotoa haina msingi kwani muda mwingi hakuweza kufanya kazi na tume hiyo. “Rajani ushiriki wake kwenye tume ni chini ya asilimia 10, muda mwingi alikuwa anasafiri au anakuwa kwenye kazi za asasi yake, mambo mengi alikuwa hajui na sisi tulikuwa kila kitu tunaamua kwenye vikao, kuna kazi tuliyompa ya kuangalia kamakila tulichojipangia kimefanyika kwa wakati, alishindwa kwa sababu muda mwingi hakuwapo,” alisema: Alisema kuwa, msimamo wa Rajaniulikuwa ni kuachana na wanafunziwaliofeli na badala yake tume ijikite kuangalia mambo mengine, jambo alilosema lilikataliwa na wajumbe wengine. “Sisi tuliona kuwa ni ukweli mfumouliotumika kupanga matokeo ulikuwa tofauti na kukaonekana kwamba ukibadilishwa matokeo yatakuwa tofauti, ndiyo maana tukasema matokeo yapangwe upya.