HADITHI



          Mwanamalundi        
    
" yasikukute ni bora uyasikie yakikukuta utalia kuliko mie'

    NA Israel Binaisa



           kwanza tuanze nakumshukuru mwenyezi mungu  muumba wa aridhi na mbingu na vitu vyote vilivyopo ndani ya dunia hii natumaini muwazima wa afya njema, ugueni pole wenye matatizo mbali mbali ya kiafya  wagonjwa wote waliopo ma hosipitalini na waliofungwa jela kwa makosa ya kusingiziwa  LIFE PARTNET ENTERTAINMENT  tunapenda kuwaleteeni  hadithi yenye mkasa wa kusisimua  kama tulivyo duniani hakuna mwanadamu hasiyependa maisha ya raha na hakuna mwanadamu anayependa shida  hadithi hii inawahusu mapacha wawili ambao walizaliwa ila hawakubahatika kupata malezi ya mama  kwani mama yao alifariki mda mfupi baada ya kujifungua watoto hao hivyo mapacha hao kulelewa na ndugu ata hivyo baba yao alifariki baada ya miezi  miwili baadae kwa kugongwa na gari  hivyo ikapelekea kufanya vichanga  hivyo kulelewa katika mazngila  magumu zaidi  vichanga hivi ni kulwa  mwanamalundi  na doto aliitwa saleh na baba yao aliitwa  malundi na mama yao aliitwa rebeca malundi ama kweli YASIKUKUTE NI BORA UYASIKIE YAKIKUKUTA UTALIA KULIKO MIE fuatana nasi upate kujua  zaidi mkasa huu ambao utaluka ijumaa na jumatatu hii ni hapa pekee luckyjurnior.blogspot.com
                                             
                                                      SEHEMU YA KWANZA 1
        Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi baada ya wazazi wao kufariki na watoto hao kulelewa na baba yao  mdogo ambaye alifahamika kwa jina la Jafety  ,baada ya miezi minne baada ya wazazi wao kufariki ugomvi ulianza kujitokeza katika familia ya bwana Jafety  ilikuwa ni saa saba usiku mama                                  JAFETY akiongea na mumewe 
     Mama Jafety;mume wangu  hivi ni nini  hatima ya hawa waatoto ?
  Jafety;kwani kuna tatizo?
    Mama jafety; tatizo lipo 
   Jafety; tatizo lipi ilo
     Mama Jafety; kwani toka tulipo oana  sijabahatika kupata mtoto ,alafu leo hii na lea watotot wa mtu mwingine tena mapacha uoni kwamba ni tatizo
    Jafety ;mke wangu kumbuka hawa watoto ni yatima tena ni watoto wa marehemu kaka yangu ,hivyo  jukumu lakuwalea ni letu sote kama wanandoa
    Mama Jaffety;hivi hawa watoto unawalea sangapi wakati ukitoka kazini unaenda moja kwa moja bar ,sasa ni nachokisema ni kwamba nimechoka  kulea  hizi mbwa zako zisizo na adabu kula mda wote kama mbwa koko
JFETY; mke wangu usiwe hivyo kuwa na roho ya kibinadamu ,na kuahidi kuwa karibu nawe mda wote  Katika kuwalea hawa watoto  
 Mama Jafety; nitavumilia kama ukifuata mashariti yangu ,ukitoka kazini naomba urudi nyumbani  na tusaidiane kulea  hawa watoto 
Jafety; ilo halina tatizo
                                  BAADA     YA     MWAKA MMOJA
         Baadae malezi ya watoto  hao yalizidi kusikitisha jamii afya zao zilizolota  kwani hawa kupata huduma za kutosha  mara nyingine walishinda na njaa na kufungiwa ndani majirani waliwaonea huruma sana watoto hao habari zilizagaa  zaidi mitaani kwa unyasaji wa hao watoto kweli mwanamke huyu bi;sauda alikuwa katiri hakuna mfano kama vile hakuzaliwa na binadamu ,kwani mda aliotaka kuondoka nyumbani aliwafungia watotot hao nakuwaacha bila msaaada wowote.
   Ndipo majirani uzarendo ulipowashinda siku hiyo asubuhi  mwanamalundi alikuwa akicheza karibu na jiko lililokuwa limepashiwa maji alilidondosha kwa bahati mbaya na maji kumchoma karibu sehemu zote za mwili wake  hakuweza kupata msaada wowote  kwani malango ulikuwa umefungwa kwa nje ,Mama Sabela ambaye ni jiran yao alishituka kusikia vilio mfululizo  alipofika  nyumbani kwa Jafety alikuta malango umefungwa kilichomshangaza zaidi alipoona  mlango huo umefungwa na kufuri huku vilio vya watoto hao kutokea ndani  humo ndipo alipoamua kwenda kutoa taarifa kwenye kituo kidogo cha polisi ata hivyo jitihada zake ziligonga mwamba  baada ya askari hao kumtaka alipe kiasi cha shiringi elfu therathini na kukodiwa gari ili waende eneo la tukio 
Mama Msamalia mwema ;tafadhari naitaji msaada wenu na pesa hiyo mnayoitaji mimi hapa sina tafadhari naomba tusaidiane kuokoa maisha ya watoto 
Afande; lakin hebu  twende tukamsaidie 
  polisi walipofika eneo la tukio  walikuta kimya kimetawala  kitu ambacho kilimpa  wasiwasi mama sabela  ndipo polisi walipo amua kuvunja mlango na kuingia ndani hali waliyo ikuta ilisikitisha zaidi na  kuhuzunisha na hakuna haliyeweza kujizuia kutoa machozi maana waliwakuta watoto hao wakiwa hawana nguo hata moja huku wakiwa wamelala sakafuni  Mwanamalundi alikuwa na hali mbaya zaidi
kwani mwili wake ulitisha kwa vidonda vilivyotawala mwili mzima 
      Askari waliwachukua watoto hao na kuwapeleka katika hospitali ya rufaa waikwa chini ya usimamizi wa mama sabela .huku polisi wakiendelea na jitihada za kuwa tafuta walezi wa watoto hao 
                                                ****
Sauda alipofika nyumbani alishangaa kuoana hali aliyoikuta mlango ulikuwa umebomolewa  na alipojaribu kuchunguza ndani hakuwakuta watoto ndipo alipo amua kumpigia simu mumewe  lakini simu ya mumewe iliiata bila kupokelewa  na ni kitu kilichozidi kumpa wasiwasi zaidi  aliamua kwenda kwa mama isabela lakini alimkosa alivyo pita katika mitaa  majirani walimtazama kwa hasira sana na  hata alipo wasalimia baadhi yao hawa kuitikia salamu yake akiwa anatafakari nini cha kufanya akakumbuka kumpigia simu mumewe kabla ajapiga simu .simu yake sauda iliita alikuwa ni mama isabela jirani yake ndiye aliyempigia 
Mama isabela;hallo 
Sauda;halo mama isabela mwenzio nina matatizo hapa nyumbani
  Mama isabela;kuna nini 
Sauda;nilikuwa nimeenda kumsalimu mama kijijini niliporudi nimekuta mlango umevunjwa na watoto hawapo
  Mama sabela; hivi shoga yangu unapotoka nyumbani watoto uwa unawaaacha na nani
 Sauda; niwaaache na nani wakati unajua hapa nyumbani  niko peke yangu ,ninacho kifanya uwa nina wafungia ndani 
  Mama sabela;shoga yangu kweli wewe ni katiri sana tena ufai 
ghafla simu ya mama isabela inaisha chaji ,mara simu ya sauda inaita kwa mara nyingine  kuitazama anakuta namba ya mumewe  anashituka kusikia sauti ya kike taarifa anazo pata zinamchanganya zaidi ,
             njoo haraka hospitali ya rufaa uweze kumuona mumeo akiwa anajiandaaa kutoka nyumbani kwake ghafla kwa mbali anaona gari ya polisi ikija kwa kasi upande wake
           
            JE NINI KILIENDELEA ENDELEA KUFUATILIA BLOG HII PEKEE
                                                  SEHEMU YA PILI
     ILIPOISHIA JUMATATU ,sauda akiwa anajiandaa kutoka nyumbani kwake kuelekea hospitali alikotakiwa kufika haraka,mala gari ya police inafunga breck mbele ya nyumba yake police wenye silaha nzito wanaluka ndani ya difender na kumvaa sauda kisha kumtupia ndani ya gari ,ungebahatika kuwaona ungedhani labda walikuja kumkamata jambazi sugu.sauda alikua akitetememeka mwili mzima kila alipouliza nini kosa lake alijibiwa kwa vibao,       

       Huko hospital hali iizidi kuwa mbaya kwa JAPHETI  kila mda ulivyozidi kwenda presha ilizidi kupanda,Mama isabera kila alipojalibu kupiga simu ya Sauda haikupatikana na kumfanya azidi kuchanganyikiwa  kwa sababu  hakukua na ndugu hata mmoja aliefika toka wafike asubuhi zaidi ya japhet ambae nae alipofika tu akazilai
                                                     *******

     Sauda alipofikishwa katika kituo kidogo cha police uyole awali alikana mashtaka yanayo  mkabiri hivyo askari hao kuamua kuongozana nae hadi hospital ya rufaa ambako Mwanamalundi alikua akitibiwa  alipofika na kuingia whod ya watoto alishangaa¡ kumuona mama isabela akiwa bize kumnywesha uji .Mwanamalundi huku mgongoni akiwa amembeba sarehe  alibubujikwa na machozi na baadae kukiri kua mwenye hatia na kwa uchungu ",alionge huku akili  nakili kua mimi ni mwenye hatia pore mama isabela kwa kuokoa maisha ya watoto hawa hivyo sina budi kusema nastail azabu inayonipasa bira kunipeleka mahakamani"
       walitizamana na mama sauda kuangua vilio ambavyo viliwashitua baadhi ya wagonjwa ,askal waliamua kumtoa nje sauda lakini kabra ya kutoka sauda aliomba awasiliane na mumewe lakini .mama isabera alimkatisha ",mumeo yupo wodi namba kumi ,! mungu wangu kafanyeje tena ,nenda kamuone akiwa kwenye koldo madacktari wawili wanatoka wodi namba  kumi huku wakibishana ***lakini tumejitaidi kuokoa maisha yake JE NINI KITAENDELE A FUATANA NASI JUMATATU  UPATE KUJUA NINI KILIENDELEA
                         SEHEMU YA TATU
       Sauda alifikishwa hosipitali akiwa chini ya ulinzi wa askari ,mama isabela alimsimulia yote hadi kupelekea mwanae kulazwa hospitali .akiwa anaelekea wodi  aliyolazwa jafety anapishana na madaktali wawili waliokuwa wakimtibu mumewe huku wakisimuliana jitihada walizo tumia kuokoa uhai wa jafety lakini ikashindikana .sauda anaingia wodini nakukuta nesi akifunika mwili wa jafety anvyotaka kufunua shuka ilikumjulia hari mumewe nesi anamshika mkono nakumvutia nje"bila shaka wewe ni ndugu wa jafety ? pole kwa haya yaliyotokea  haya mambo yapo na yanatoke hivyo  hunabudi kufunga mkanda na kujikaza " sauda ambaye kwa mda huo alionekana kuwa na wasiswasi mwingi huku machozi yakimtoka nguvu taratibu zilianza kumuishia  kwani alianza kufungua na kujua kuwa jafety mumewe tayari ameshapoteza maisha  ata hivyo alisaidiwa na polisi ambao walikuwa naye  na kimtoa nje ya wodi .Dactari ambaye alikuwa akimtibu mumewe   aliwafuata na kuwapa taarifa rasmi za kifo cha jafety .Mama isabela anapata wakati mgumu zaidi  hivyo anahamua kuwa pigia simu ndugu wa jafety 
                      ****************
Ilikuwa ni asubuhi na mapema ndugu wanakusanyika nyumbani kwa jafety ,majirani wa shitushwa na kifo cha jafety  ,awali walijua kuwa mwanamalundi ndiye aliyefariki,mwili wa jafety unapelekwa nyumbani kwake kwa ajiri ya taratibu za mazishi kuendelea .Ni siku ya tatu toka jafety afariki huku mkewe akiwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la unyanyasaji wa watoto,Jafety alizikwa katika makaburi ya Itolowa 
     Siku ya nne ndugu wanakaa kikao na kumuomba mama Isabela kuwasimulia yaliyotokea kila mtu anasikitishwa na taarifa aliyotoa mama Isabela ,mzee mmoja wa makamo  anasimama na kumpongeza mama isabela ,na kuwaomba wakina mama kuiga mfano wa mama huyo ,wanatoka baadhi ya ndugu na kuongozana na mama isabela  hadi hosipitari alikolazwa mwanamalundi walipofika hosipitali  walisikitishwa na hali waliyo mkuta nayo mwanamalundi baadae wanapanga mipango jinsi ya kuwalea watoto hao ,dada wa marehemu mama justina  anajitokeza nakuomba mwanamalundi na salehe wawe chini yake na kuishi nao .Ndugu wanakubali bila kipingamizi 
      Baada ya miezi miwili mwanamalundi na salehe  wanarudi katika hali nzuri na kuishi maisha ya furaha ,mama Isabela anajijengea utaratibu wakuenda kuwaona watoto hao kila mwisho wa wiki ,mama Isabela anafurahi sana 
        Siku moja mama Isabela akiwa anaelekea nyumbani kwakina Mwanamalundi anashangazwa na hali aliyoikuta nyumbani hapo
ukimya ulitawala  uliomfanya mama Isabela amini hakukuwa na mtu nyumbani hapo .alibisha hodi lakini hakuwepo mtu wa kuitikia na hivyo akaamua kwenda kwa jirani kuwaulizia  alimkuta kijana mmoja alipouliza alijibiwa kwamba  shangazi wa mwanamalundi amesafiri ila wao uwa wanabaki na dada yao  shangazi aliondoka 
                     **************************
           Ilikuwa ni siku ya  furaha kwa sauda kwani alikuwa amemaliza kifungo chake gerezani hivyo aliachiwa huru .Alirudi nyumbani kwaajiri ya kuanza maisha upya uku asijue ni wapi kwa kuanzia alienda kwa mama Isabela na mama Isabela alifurahi sana kumuona Sauda
Mama Isabela; "ndugu yangu pole kwa matatizo                                         
 Sauda: asante nashukuru,za hapa nyumbani
Mama Isabela alimtizama sauda bila atakumaliza  sababu sauda alionekana kachoka na ngozi yake maji yakunde ilibadilika  na kuwa ya kaawia na vipele vidogo vidogo vilivyo tanda karibu mwili mzima pia alionekana kupungua mwili na kuwa mnyonge na mwenye mawazo mengi sana kwa kifupi alitia huruma
 Mama Isabela alimkaribisha ndani na walianza maongezi Sauda alimsimulia yote maisha ya gerezani na pia mama Isabela nae alimsimulia  yote yaliyo tokea toka kifo cha mumewe na kumfanyaSauda kutokwa na machozi kilichomumiza zaidi ni pale alipopewa taalifa ndugu wa Jafeti kuuza nyumba yao na mali zote walizochuma na mumewe sauda aliuliza "hata hoteli"
alijibiwa ndiyo kwani msiba ulipoisha vitu vyote vilipigwa mnada
hata ile gari yangu ?
          
                                SEHEMU YA NNE
Sauda alizidi kuchanganyikiwa baada ya kupewa taarifa kua ndugu wa mume wake wamepiga mnada mali zote walizochuma na mumewe  pamoja na gari ya sauda aliyoinunua kwa pesa yake mwenyewe  
    Akiwa katika dibwi la mawazo aliyakumbuka maisha yake ya zamani jinsi alivyokuwa akijirusha katika viwanja mbali mbali roho ilimuuma sana pale alipokumbuka kwamba alipotaka kwenda kwenye starehe watoto aliwafungia ndani bila hata msaada wowote na alipomaliza mizunguko yake ndipo aliporudi nyumbani pia aliumia sana alipokumbuka siku ile ambayo ndiyo chanzo cha matatizo yote na kupelekea kifo cha mumewe Sauda alitamani kurudi nyumbani lakini kwa jinsi alivyokuwa akimtendea mama yake alipokwenda kumsalimu alikata tamaa maana alimfanyia kitendo cha kinyama sana alifikiria sana ila hakupata jibu "hivi leo hii sauda mimi  ndiyo wakuwa hivi ama kweli dunia kigeugeu  niliwadharau wazazi wangu  ni miaka tisa tangu niolewe lakini sijawai kuwatembelea mbaya zaidi nilimkana mama yangu mbele ya rafiki zangu pia sikupenda kushirikiana na majirani zangu kwa sababu hari ya maisha yao na mimi niliamini hatufanani 
  Sauda alishitushwa na mama isabela ambaye alikuwa kimya mda wote utadhani alijua alichokuwa anawaza Sauda
  Mama Isabela ; sauda punguza mawazo mdogo wangu haya mambo yako na yanatokea cha kufanya rudi nyumbani  kawaombe radhi wazazi wale ni watu wazima watakuelewa
 ****************************************************
            Nyumbani kwakina mwanamalundi  siku hiyo  ilitawaliwa na huzuni bila kikomo kwani hadi sasa  saa mbili usiku mwanamalundi na saleh hawa kueleweka wapi  waliko majirani waliwatafuta kwa mda mrefu bila kupata mafanikio hivyo iliwabidi kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa  ilikuwa ni saa tano usiku shangazi yao alilia sana na kusema  hivi nini kimewapata wanangu na nitasema nini kwa ndugu zangu .pamoja na mawazo yote  kumbe sababu ya watoto hao kuondoka nyumbani ni kwamba shangazi yao alipokwenda kazini wao alifanyisha kazi ngumu na siku nyingine walinyimwa chakula na hiki ndicho chanzo cha watoto hao kutangatanga mitaani na baadae kutoloka nakuwa watoto wa mitaani 
                     ********************************
    Mvua kubwa ilinyesha ilikuwa imeambatana na  upepo mkali pamoja na ngurumo za radi  Mwanamalundi pamoja na Sarehe walikuwa chini ya mti mkubwa ambapo walikuwa wamejihifadhi kwa usiku ule baada ya maangaiko  ya siku nzima walijikunyata  wakiwa wana tetemeka baridi kali  ghafla walishitushwa na mwanga mkali uliokuwa umeelekezwa walipo lala  waliaanza kukimbia na kila mmoja asijue mwenzie wapi alikoelekea 
                   ***************************
Nyumbani shangazi wa mwanamalundi aliendelea kuwataarifu ndugu kwa kutumia simu yake ya mkononi  ghafla alisikia mlango ukigongwa  aliamka taratibu  na kuenda mlangoni alipofika mlangono alisikia sauti za vilio zikisikika kwa mbali  sana  alipojaribu kuuliza ni nani ,sauti ilizidi kuongezeka  aliposikiliza kwa makini aliitambua sauti akafungua mlango taratibu alipomaliza tu kuufungua ule mlango  alishituka kuona kuwa ni  Sarehe  na hali aliyokuwa nayo siyo ya kawaida  alipomuuliza mwenzake  alipo kabla hajajibiwa   mala walisikia kilio "mama nakufaaaaaa " kikitokea mbali kidogo na kilisikika mara mbili tu  na ghafla kukatawaliwa na ukimya 
              JE NINI KILITOKEA USIKOSE KESHO JUMATATU

No comments:

Post a Comment