Saturday 25 May 2013

‘ASILIMIA 31 YA WATANZANIA NI WALEVI.'

Dodoma. Asilimia 26.8 hadi asilimia 31.9 ya Watanzania wanatumia pombe na asilimia 27.4 kati ya hao ambao ni wanaume na wengine asilimia 13.4 ambao ni wanawake, ni walevi wa kupindukia. Bunge lilielezwa jana. Takwimu hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, ambaye alisema kuwa viwango hivyo vimetokana na utafiti uliofanywa kati ya Februari hadi Oktoba mwaka jana 2012. Kwa mujibu wa naibu waziri, utafiti huo ulifanywa na Shirika laAfya Duniani (WHO). Alikuwa akijibu swali la Abdallah Haji Ali (Kiwani–CUF) aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu utumiaji wa pombe ambao umethibitika kuwa ni hatari kwa afya za binadamu. Pia alipendekeza pombe ipigwe marufuku kabisa hapa nchini kwa kuzingatia madhara yake. Naibu waziri alisema tafiti zimeonyesha kuwa watu milioni mbili wanafariki dunia kila mwaka duniani kutokana na madhara ya matumizi ya pombe na asilimia nneya matatizo ya kiafya yanatokana na matumizi ya pombe. “Hali inazidi kuwa mbaya zaidi katika nchi zinazoendelea hasa kutokana na kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi na ustawi wa jamii inayochangiwa na magonjwa ya malaria, kifua kikuu na Ukimwi,” alisema Dk Rashid. Naibu Waziri alisema kutokana na kuongezeka kwa athari zitokanazo na matumizi ya pombehasa kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Serikali inatekeleza mkakati wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukizwa unaoelekeza kutoa elimu kwa wananchi kupitia njia mbalimbali. Kuhusu mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo, alisema tayari Serikali imeanza utaratibu wa kuziwezesha hospitali za rufaa zamikoa, kuanza kutoa huduma kwawaathirika wa matumizi ya dawa za kulevya na pombe.

SAKATA LA GESI MTWARA: WABUNGE WA CCM WACHARUKA.

Dodoma. Wabunge wa CCM wamekuja juu na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi vigogo wa Serikali mkoani Mtwara, wakiwamo Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kutokana na kile walichoeleza ni uzembe uliochangia vurugu zinazoendelea za wananchi kugomea gesi kutoka nje ya mkoa huo. Wengine waliopendekezwa kuchukuliwa hatua ni kamati nzima ya ulinzi na usalama ya ngazi ya mkoa na wilaya ya Mtwara mjini, wakiwamo makamanda wa polisi. Kutokana na hali hiyo, vigogo kadhaa mkoani humo wako hatarini kukumbwa na ghadhabu hiyo akiwamo Mkuu wa vikosi vyaJeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mkuu wa mgambo na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Wabunge hao walikuwa wakitoa mapendekezo hayo kwenye kikaocha Kamati ya Wabunge wa CCM iliyofanya kikao cha dharura juzi usiku, mjini hapa. Kikao hicho kiliongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, huku Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye wakati huo alikuwa kwenye kikaocha Kamati ya Uongozi wa Bunge,aliwakilishwa na Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama. Katika kikao hicho maalumu kilichokusudia kutoa ushauri kwa Rais Kikwete juu ya njia mwafakaya kutatua hali ya machafuko, wabunge wengi wali kukasirishwa na jinsi hali ilivyo mkoani Mtwara. Chanzo chetu kwenye kikao hichokilieleza kuwa wabunge hao walichukizwa na jinsi Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya walivyokuwa wakipingana kimsimamo. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Joseph Simbakalila, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Wilman Ndile na Kamanda wa Polisi Mkoa Linus Sinzumwa wamehusishwa. Licha ya baadaye kuonekana kuwa kitu kimoja, wabunge hao walidai kuwa walishindwa kutumianafasi zao katika kutatua tatizo hilo, ambalo hadi juzi Serikali ilisema walikuwa wamekufa watu watano, wakiwamo wanajeshi wa JWTZ waliofariki katika ajali wakati wakienda kutuliza machafuko. Chanzo hicho kilieleza kuwa iwapomapendekezo ya wabunge hao yatapelekwa kwa Rais Kikwete kama michango ya wabunge hao ilivyokuwa, huenda rungu likawaangukia pia viongozi wa kisiasa wa CCM mkoani humo. Miongoni mwa wanasiasa hao, chanzo hicho kimesema ni wale waliotoa kauli za waziwazi kuungamkono msimamo wa kutoruhusu gesi kusafirishwa nje ya mkoa huo. “Hapa wapo wabunge, madiwani na viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM,” kilieleza chanzo hicho. Hata hivyo, baadhi ya wabunge walipendekeza mkakati wa kutatua uzembe uliofanyika Mtwara, unapaswa kuchukuliwa kwa uangalifu usije ukasababisha madhara mengine kwa Chama na Serikali. Walisema suala hilo halina budi kuchukuliwa kwa uangalifu hasa ikizingatiwa kuwa Chama cha CUF ndicho chenye nguvu mkoani humo ukilinganisha na vyama vingine vya upinzani. Wabunge hao walikituhumu chamahicho kuwa kimekuwa kikijaribu kutumia vurugu hizo kama kigezocha ushawishi wa kukubalika mkoani humo.